Wednesday, May 23, 2012

JINSI MALARIA INAVYOONGOZA KWA KUUA TANZANIA


Malaria yaongoza kwa kuua

23rd May 2012
Chapa
Maoni
Wagonjwa wa Malaria
Ugonjwa wa malaria umetajwa kuwa bado ni tishio nchini kutokana na kuongoza kwa kuua watu kati ya 60 hadi 200 kila siku.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya mkoa wa Mwanza Sekou Toure, Dk. Onesmo Wakyedela, alitoa takwimu hizo jana na kuongeza kwamba takwimu zilizopo katika hospitali ya Sekou Toure zinaonyesha kuwa watoto chini ya miaka mitano ndio wanaofariki zaidi kutokana na malaria.
Kwa mujibu wa Dk. Wakyedela, mwaka 2011 asilimia 39 ya watu waliokufa kutokana na ugonjwa wa malaria  ni watoto, na kwa upande wa watu wazima walikuwa asilimia 25.
Mganga Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Dk. Valentino Bhangi, alisema kuwa tiba sahihi na ya mapema ni njia sahihi ya kupambana na malaria na kuwashauri wagonjwa kufika hospitali kila wanapohisi dalili za kuumwa.
Meneja wa Benki ya Stanbic, Joshua Kyelekule, ambaye benki yake ilitoa msaada wa vyandarua 350 kwa hospitali hiyo, alisema  benki yao inatimiza wajibu wa kutoa misaada katika sekta ya afya ikiwa ni sehemu ya makubaliano kati yao na Shirika la Afya Duniani (WHO).


No comments:

Post a Comment