Wednesday, December 23, 2015

FAIDA ZA KUNYWA MAJI ASUBUHI









UNYWAJI WA MAJI

Katika mwili wa binadamu, unywaji wa maji husaidia siyo tu kuondoa kiu anayokuwa nayo mtu, bali pia maji husaidia kufanya kazi mbalimbali katika mwili ikiwa ni pamoja na kutuepusha dhidi ya magonjwa mbalimbali.
Maji huchukua karibu asilimia sabini (70%) ya mwili wa binadamu, ambapo seli za ubongo zina karibu asilimia themanini na tano (85%) ya maji, misuli huwa na asilimia sabini na tano (75%) ya maji, mifupa huwa na asilimia ishirini na tano (25%) ya maji na damu huwa na karibu asilimia themanini na mbili (82%) ya maji.
Watu wengi tunayo mazoea ya kunywa maji pale tunapojisikia kufanya hivyo, ila kiafya miili yetu huhitaji maji muda wote. Tunapokunywa maji muda wa asubuhi tunapoamka, tunapata faida zifuatazo:
  • Kunywa maji asubuhi kabla hujala kitu chochote, huwezesha utumbo kufyonza chakula vizuri na kufanya virutubisho viingie mwilini kwa urahisi.
  • Husaidia ukuaji wa ngozi yenye afya kwani maji huwezesha sumu mbalimbali zilizoko kwenye damu zitoke mwilini.
  • Kunywa maji asubuhi husaidia kuweka uwiano katika kinga ya mwili na hivyo kuuwezesha mwili kupambana na magonjwa na kukupa uwezo wa kufanya kazi zako siku nzima.
  • Maji yanaponyweka asubuhi huwezesha seli mpya katika misuli na damu kutengenezwa kwa haraka zaidi na kuzidi kukufanya kuwa na afya imara.
  • Unywaji wa maji asubuhi imegundulika kuwa husaidia kuondoa matatizo kama vile kuhisi kichefuchefu, matatizo ya koo, matatizo ya macho, matatizo ya tumbo kama kuharisha, matatizo ya figo, mkojo, matatizo ya kupata maumivu ya kichwa na mengine mengi.

Ili kuweza kupata matokeo mazuri kiafya kwa kunywa maji asubuhi, ni vizuri ukazingatia yafuatayo:
 Kwanza ni kuhakikisha muda wa  saa moja kabla ya kunywa maji uwe hujala kitu chochote na pia baada ya kunywa maji, subiri kwa muda wa saa moja ndipo ule chakula. 
Pili ni kuhakikisha kuwa kiwango cha maji utakayokunywa ni sawa na lita moja na nusu yaani sawa na glasi sita, ni ngumu kunywa kama mtu ndiyo unaanza lakini kadri siku zinavyoenda mwili utazoea na unaweza kuanza kwa kunywa glasi tatu za maji ukapumzika kama muda wa dakika kadhaa halafu ukamalizia glasi nyingine tatu zilizobaki. 
Jambo la tatu ni kwamba, uwe hujatumia kinywaji chenye kilevi usiku, kwa maana kwamba isije ikawa usiku umetumia kilevi halafu asubuhi ukategemea unywe maji na kupata matokeo sawa na mtu ambaye hakutumia kinywaji chenye kilevi au pombe.
Maji ni kwa ajili ya afya na uhai wetu, tujenge mazoea ya kunywa maji yanayotosheleza mahitaji ya miili yetu. Kwa siku kunywa lita mb

“KUNYWA MAJI KWA AFYA YA MWILI WAKO"

ili mpaka tatu za maji husaidia kuuweka mwili katika hali nzuri kiafya.

No comments:

Post a Comment