Wednesday, December 23, 2015

Maradhi ya Bawasiri ,Mgolo, Mjiko (hemorrhoids)

MARADHI YA BAWASIRI, MGOLO MJIKO 
(Hemorrhoid)
1) Maradhi ya bawasili, mgolo, mjiko
 Maradhi haya hushambulia njia ya haja kubwa. Hujitokeza kwa sura tofauti na hali tofauti. Kwa hapa Tanzania na Afrika Mashariki kwa jumla, aina tatu za maradhi haya ni maarufu sana na yamekuwa yakiwaumiza watu wengi. Katika makala hii nitazitaja aina hizi tatu:
i) Kutoka kinyama katika njia ya haja kubwa
Kuna vinyama vya aina mbili. Cha kwanza ni kirefu hutoka ndani ya njia ya haja kubwa baada ya haja kubwa au mtu anapochutama. Kwa lugha ya kitaalam huitwa skin tab. Cha pili ni kinyama kinachoota pembezoni mwa mzunguko wa njia ya haja kubwa. Kwa kitaalam hiki huitwa external hemorroid . Hizi ni aina mbili za vinyama vinvyoota njia ya haja kubwa.
ii) Mpasuko katika njia ya haja kubwa
Walio wengi hupata maradhi haya. Njia ya haja kubwa hufanya mchaniko pembeni (anal fissure). Mchaniko huu husababisha maumivu makali sana hata mtu hushindwa kukaa. Mara kwa mara hutoa damu hasa mtu anapojisaidi haja kubwa. Maumivu makali hupatina.
iii) Kushuka nyama kubwa njia ya haja kubwa
Baadhi ya walio wengi hushukwa na nyama katika njia ya haja kubwa. Baadhi ya watu wa pwani hasa visiwani huliita nyama hili ni futuru. Hii ni moja ya aina ya maradhi ya bawasili, mgolo, mjiko.
Kwa kuwa hizi ni aina muhimu zinasosumbua sana hapa ukanda wa pwani wa Afrika Mashariki naomba tuishie hapo. Mungu akipenda siku nyingine utaangalia maradhi mengine


2) Sababu za maradhi ya bawasili (mgolo, mjiko)
Zipo sababu kuu sita za maradhi haya nazo ni:
a) Kuinua vitu vizito (kujikamua)
b) Kukaa kitako (kukaa chini) muda mrefu (mkandamizo wa njia ya haja kubwa)
c) Kujikamua sana wakati wa haja kubwa: hasa kwa wanaopata choo kigumu (constipation)
d) Kuharishamuda mrefu
e) Kuzaa
f) Kuingiliwa kinyume na maumbile hasa uume ukiwa mkubwa kuliko njia


3) Athari za maradhi haya
Mambo yafuatayo hujitokeza kwa mtu ambae anasumbuliwa na maradhi haya
i) Huwa hana hamu ya endo la ndoa (kwa mwanamke na hata kwa mwaname)
ii) Mwili huwa unachoka sana hasa alfajiri
iii) Mwanamme humaliza haraka tendo la ndoa (hufika kileleni haraka sana) kabla mwenza hajakolea
iv)Sehemu za nyuma huwasha (baadhi ya watu)
v )Kiuno huuma na hukaza sana
 Wengine huumwa na miguu


 MATIBABU NA JINSI YA KUEPUKA TATIZO LA BAWASIRI

~matibabu ya bawasiri hutegemea na Aina ya bawasiri pia tiba iliyozoeleka ni kukatwa kinyama na kuendelea na lishe ya chakula hata hvyo tiba hii si nzuri kwasababu huwa haitibu chanzo cha tatizo hivyo huwa rahisi kujirudia hivyo tiba nzuri ni kutumia dawa na anion chip kubandika mahali penye tatizo na kuondoa tatizo Hilo
~Pamoja na hayo bawasiri ni ugonjwa unaoweza kuepukika kwa kuzingatia
��KULA MBOGAMBOGA ZA MAJANI, MATUNDA, NA NAFAKA ZISIZOKOBOLEWA
��KUNYWA MAJI MENGI ANGALAU GRASS 6-12 Kwa siku
��EPUKA KUKAA CHOONI KWA MUDA MREFU
MADHARA YA TATIZO LA BAWASIRI
��kupata upungufu wa damu (anemia)
��Kupata tatizo la kutokuweza kuhimil choo
��hupunguza nguvu za kiume na kuondoa hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake


Wahi hospitali mapema 
Bawasiri inatibika
More contacts lizshayo@gmail.com

No comments:

Post a Comment